RAIS Samia Suluhu Hassan amempisha Georgina Magesa – Miaka 8, na kumruhusu akae kwenye kiti chake.
Mama Samia alifikia hatua hiyo baada ya kuona Makala fupi ya mtoto huyo iliyorushwa na Azam akielezea ndoto zake za kutamani kuwa Rais wa Tanzania siku moja.
“Ni katoto…kajukuu ka Kiafrika…ambako kana mtazamo wa mbele na mtazamo mkubwa. Kameanza kazi ya kuandika vitabu kwa umri ule…Mungu amkuze…Mungu amnyooshee afike pale anapotaka…” Rais Samia akitoa baraka kwa mtoto Georgina Magesa.